Mama alivyopeleka hili gari mpaka baharini kwa makusudi huku watoto wakipiga kelele ‘mama anatuua’
Hii imetokea Marekani ambapo mama huyu mwenye umri wa miaka 32 akiwa ni mjamzito, aliamua kuliendesha gari hili na kuliingiza kwenye bahari kwa makusudi huku watoto wake wakipiga kelele kwamba mama anajaribu kutuua.
Watoto wa Mwanamke huyu ambae imeripotiwa kwamba bado yuko hospitali
akifanyiwa vipimo vya matatizo ya akili, ambao wana umri wa miaka
mitatu, tisa na 10 walichukuliwa na Idara ya watoto na familia kwenye
jimbo la Florida baada ya kupata matibabu.
Watoto hawa wote walikuwemo kwenye gari hili lililolengeshwa baharini
na mama yao ambae anadai alikua anakwenda kwenye sehemu salama ambayo
mume wake walieachana asingeweza kuwafata au kujua waliko.
Wakati
hili tukio linatokea alikuepo karibu Mtalii raia wa Canada ndio maana
video ya tukio na hizi picha zimepatikana zikionyesha kila kitu.
No comments:
Post a Comment