Bunge la Libya lamuondoa madarakani Waziri Mkuu

Meli inayoidaiwa kutokomea
Bunge la Libya limemuengua madarakani 
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan, baada ya vikosi vya nchi hiyo 
kushindwa kuzuia kutoroka kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya mafuta 
huku ikipeperusha bendera ya Korea ya Kaskazini. Jumla ya wabunge 124 
kati ya 194 waliohudhuria bungeni Jumanne ya jana waliidhinisha kura ya 
kutokuwa na imani kwa wingi wa kura zaidi ya kiwango kinachotakikana na 
hivyo kuweza kumuondoa madarakani Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan.
Wakati huohuo bunge hilo la Libya 
limemteuwa Waziri wa Ulinzi Abdullah al Thani kuwa Waziri Mkuu wa Mpito,
 na hivyo bunge hilo kuwa na muda wa wiki mbili wa kutafuta shakhsia 
mwingine atakayechukua nafasi ya Zeidan. Itafahamika kuwa, wanamgambo 
wanaoidhibiti bandari ya Sedra huko mashariki mwa Libya, Jumamosi wiki 
hii walipakia mafuta kwenye meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Korea ya 
Kaskazini kwa jina la "Morning Glory" ambayo ilitia nanga kwenye bandari
 hiyo bila ya kibali cha serikali.
Chanzo, tehranswahili.com (R.M)
No comments:
Post a Comment