TANZANIA KUWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI KOREA
Spika wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Anna makinda akimweleza mwaenyekiti
mwenyekiti wa mambo ya nje na muungano kutoka Korea Bw Ahn Hong Joon
mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea
ikiwemo ufunguzi wam ubalozi wa Tanzania nchini Korea wakati wa kikao wa
kikao kilichofanyikamapema leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon
akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna
Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala
yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza
jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw.
Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo
Mjini Dodoma.
Wajumbe
wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao
kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza
jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw.
Ahn Hong Joon (hayupo pichani)
Spika Makinda alisema kuwa serikali itaendelea kulisimamia suala hili ikiwa ni njia moja wapo ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
"Tuna kila nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania nchini Korea na hii tunafanya tukiwa na nia ya kuendelea kuujenga uhusiano kati yetu" Alisema Spika Makinda.
Aidha Spika Makinda alisema kuwa bunge la Tanzania limeweka mikakati mbalimbali ili kuliimarisha na kulifanya kuwa la kimataifa ikiwamo kuridhia uanzaji wa bunge la kimtandano (E-parliament).
Akizungumzia kuhusu uanzishaji wa Radio ya Bunge Spika Makinda spika alisema kuwa bunge linampango wa kuwa na Radio ya bunge ili kupunguza gharama za kutumia radio za taifa kama wanavyofanya sasa.
Pia Spika Makinda alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon kushirikiana katika kuanzisha chama cha ushirikiano cha wabunge wa Korea na Tanzania.
No comments:
Post a Comment