Wamerekani wengine wanunua hisa Manchester United
Kampuni
moja ya uwezekazaji ya kimarekani imefanikiwa kununua robo ya hisa zote
za klabu ya Manchester United zilizowekwa sokoni katika soko la hisa la
New York.
Kampuni ya Baron Capital imekuwa ikinunua hisa kwa muda sasa na mpaka
kufikia jana ilifanikiwa kutimiza 24% ya hisa zote zilizokuwa zikiuzwa
na familia ya Glazer, inayomiliki asilimia nyingi kwenye klabu hiyo.
Kutokana na ununuzi huo wa hisa, kampuni hiyo sasa inamiliki 2.5% ya
klabu ya Manchester United.
Baron Capital imelipa kiasi cha $150million ili kuweza kumiliki hisa 9,581,636.
No comments:
Post a Comment