Ridhiwani Kikwete aanza kupiga hesabu za bungeni
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete.
Bagamoyo. Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete ameanza kujinadi akisema
endapo ataingia bungeni, atawaelimisha wabunge juu ya kuweka mbele
maslahi ya Watanzania badala ya kulalamikia posho.
Ridhiwani ambaye juzi alithibitishwa
na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea wa jimbo hilo lililowahi kuongozwa na
baba yake, Jakaya Kikwete alisema kitendo cha kutumia muda mwingi
kubishania kanuni na wengine kulalamikia posho kinatia aibu kwani
Watanzania wanahitaji Katiba Mpya.
Alisema hayo jana alipozungumza na
waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa jimbo
hilo katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Ridhiwani alisema, ikiwa atapata fursa
ya kuingia bungeni, atawaelimisha wabunge wa Katiba ili waweze
kuangalia maslahi ya wananchi kwanza na si kugombea posho.
Alisema, kitendo kinachotokea kwenye
Bunge Maalumu la Katiba cha wajumbe kugombea posho kinatia aibu, hivyo
basi wanapaswa kuelimishwa, ili waweze kujua wajibu wao.
Ridhiwani alisema kinachoonekana katika Bunge hilo ni kutunishiana misuli na si kuangalia maslahi ya wananchi,
Kutokana na hali hiyo, alisema wajumbe hao wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo na kuangalia maslahi ya wananchi.
waliowawakisliha pale, na si kuangalia mambo yao binafsi, jambo ambalo linaweza kuongeza migogoro.
Chanzo, mwananchi (R.M)
No comments:
Post a Comment