SITTA NA BUNGE LA MARIDHIANO
Mjumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta (kulia) akipongezwa na Mjumbe
Edward Lowassa baada ya kujieleza kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Bunge
hilo. Uchaguzi huo ulifanyika jana na Sitta alishinda. (Picha na Mroki
Mroki).
MWENYEKITI
mteule wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta ameonesha wazi kuwa ataongoza
Bunge hilo kwa maridhiano, baada ya kueleza kundi lililokuwa nyuma yake
wakati wa kampeni.
Miongoni
mwa wajumbe wa kundi hilo ni mashekhe, maaskofu, wajumbe wa Bunge
Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar na wajumbe kutoka kundi la 201, ambao
wameteuliwa na Rais.
Mbali na
kundi hilo, pia Sitta ameweka bayana kuwa taarifa kwamba alikuwa na
msuguano na mmoja wa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kupitia CCM, Andrew
Chenge, si za kweli kutokana na historia yake na Mwanasheria huyo Mkuu
wa Serikali wa zamani.
Hata
hivyo, wakati akiweka wazi nyuma ya kampeni na ushindi wake, kulikuwa na
wajumbe kutoka makundi makubwa katika Bunge hilo, na kwamba hata CCM
ilimkubali kwa kauli moja, ametangaza kuwa atawashughulikia wajumbe
wenye nia ya kuvunja Muungano.
Sitta
aliyechaguliwa jana kwa kura ya siri na wajumbe hao na kuibuka na
ushindi wa asilimia 86.5 ya kura zote zilizopigwa, pia aliweka wazi kuwa
atageuza sura mbaya ya Bunge hilo katika jamii, kwamba ni Bunge la
posho na kuwa Bunge la kazi ambayo itawaridhisha wananchi kiasi cha
kuwakubalia wapate kiinua mgongo.
“Nitawapenda
wote nitakaowasimamia na tutamaliza Katiba katika muda uliopangwa na
wananchi wajue hatupo hapa kwa posho na nitawasimamia hata tukiondoka
hapa, tuondoke na kiinua mgongo,” alisema.
Muungano
“Humu
ndani kuna vichwa ambavyo Rais (Jakaya Kikwete) amewateua na kila aliye
humu ni kiongozi, isipokuwa kuna wachache ambapo tumeshawaona na kwa
kujua msimamo wangu juu ya Muungano, wanataka uvunjike … miye kwa busara
tutawashughulikia ipasavyo. “Tayari hao wameshasambaza tangu jana
(juzi) taarifa kuwa nimezimia naumwa, wajue nitawashughulikia humu ndani
ya Bunge,” alisema Sitta.
Muda
Akiomba
kura za wajumbe, Sitta alisema yeye ni muumini wa viwango na kasi, hivyo
ataliendesha Bunge kwa viwango bora na kasi ya kupatikana Katiba kwa
wakati uliopangwa.
Akijibu
swali la Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora aliyehoji katika maelezo ya
Sitta anaeleza ataendesha Bunge kwa kasi na viwango, Sitta alisema;
“viwango na kasi ni falsafa yangu ya kufanya kazi …wananchi watatuelewa
Katiba ikiwafikia katika muda uliopangwa.”
Alisema
akiwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, hatokuwa na upendeleo, mtetezi hodari wa
shughuli zote zinazowafanya wajumbe wakae vizuri wawapo Dodoma na
kusimamia kanuni.
*Usiri, uwazi
Kabla ya
kuanza kupigiwa kura, Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde katika
swali lake kwa Sitta, alisema: “Bunge tunakwenda kuandika Katiba mpya na
kuna makundi mbalimbali na mwenendo wa kupitisha kanuni hasa vifungu
vya 37 na 38 tumeona kutofautiana, sasa endapo katikati ya mchakato
tukashindwa kuelewana na ikaelekea Bunge kuvunjika utafanyaje?”
Sitta
alijibu: “Mungu aepushie mbali kushindwa kuelewana hadi Bunge livunjike,
Watanzania hawatarajii kufikia huko…kwa msaada wa Mwenyezi Mungu
nitajitahidi tupate Katiba.”
Sitta
mwenye miaka 72 ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 29 na waziri kwa miaka
14, alisema kumrejesha kwenye kiti hicho cha kuwa Mwenyekiti wa Bunge ni
sawa na kumrejesha chura kwenye dimbwi la maji alilolizoea ambapo
ataogelea bila matatizo.
Baada ya
kumaliza kutoa neno na kujibu maswali ya wajumbe, Sitta alirudi katika
kiti chake, lakini kabla ya kukaa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward
Lowassa, alinyanyuka katika kiti chake na kwenda kumpongeza kwa kumshika
mkono.
Bunge la Maridhiano
Baada ya
kuchaguliwa, Sitta alitangaza kwamba hana uhasama na aliyekuwa akiwania
kuteuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo, Andrew Chenge.
Akitoa
shukrani baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo kwa kura kwa 487 kati
ya 563, Sitta alisema familia yake na ya Chenge ni marafiki wa karibu
ila wamekuwa wakichonganishwa na wapambe.
“Kweli
wapambe ni nuksi, kumekuwa na maneno kwamba tulikuwa na mchuano mkali
ndani ya CCM na tena wa uhasama, jambo ambalo sio kweli,” alisema Sitta.
Sitta
alisema wakati akiwa Waziri wa Sheria mwaka 1993, ndiye aliyempendekeza
Chenge kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Rais wa Awamu ya Pili, Mzee
Ali Hassan Mwinyi pamoja na Felix Mrema kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Alisema
tangu wakati huo wamekuwa na uhusiano wa karibu, lakini kwa vile wapambe
ni nuksi, ili mambo yao yaenda vizuri, lazima wavumishe mambo ambayo
alisema sio mazuri.
Chenge
Sitta
baada ya kuchaguliwa alisema ataandaa hotuba ambayo itaeleza mikasa ya
mchana na usiku wakati wa kampeni yake ya kuwania nafasi hiyo ya
uenyekiti, lakini alikiri kuwa alikuwa na timu nzito ya mashekhe,
maaskofu, watu kutoka Zanzibar na watu wa rika mbalimbali kutoka kundi
la wajumbe 201.
Alisisitiza
kuwa atakuwa Mwenyekiti ambaye atahakikisha Katiba itakayopatikana
inawatetea wanyonge na Katiba ambayo itailazimu Serikali ijayo kutunga
sheria ambazo zitaondoa dhuluma ndani ya jamii na itatoa haki kwa
wakulima, wavuvi na watu ambao hawana sauti.
Mpinzani
wake Hashimu Rungwe alipata kura 69 na kura saba ziliharibika. Rungwe
akitoa shukrani aliwaeleza wajumbe hao kuwa wale ambao hawakumwamini
anaamini siku nyingine watamwamini na watampa kura za kutosha.
Sitta kwa
upande wake alimshukuru Mungu kwa kumfungulia milango ya uongozi ndani
ya Bunge hilo: “Naamini kuwa Mungu ndiye anayefungua milango ya uongozi,
kwani mtu akilazimisha anaweza kupitia dirishani jambo ambalo sio
jema.MWENYEKITI mteule wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta ameonesha wazi
kuwa ataongoza Bunge hilo kwa maridhiano, baada ya kueleza kundi
lililokuwa nyuma yake wakati wa kampeni.

kwani mtu akilazimisha anaweza kupitia dirishani jambo ambalo sio jema.
CHANZO:HABARILEO
No comments:
Post a Comment