Taarifa za Mtumbwi uliozama Mtwara March 13 ukiwa na kina mama wauza samaki.

Taarifa
 kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi ni kuhusu 
Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda
 ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria 
waliokuwepo.
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa 
matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa 
mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama 
3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na wahusika 
wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi 
ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka kutafuta 
samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi 
ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria 
wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment