Kosa lililofanya mlinzi wa Rais Obama kuachishwa kazi saa kadhaa zilizopita

Jarida
 la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari watatu 
ambao ni walinzi wa president wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa 
nyumbani ili uchunguzi ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli
 moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda kwa ajili ya mkutano wa mambo 
ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi 
kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi 
kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha 
Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa 
nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.
No comments:
Post a Comment