Washiriki shindano la Maisha Plus waingia kijijini rasmi


Ofisa 
Mtendaji wa Kampuni ya dMb ambao ni wamiliki wa Maisha Plus, Masoud Ally
 (Masoud kipanya kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kijiji cha Maisha
 Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza 
kukabiliana na changamoto za maisha kuwania shilingi milioni 25 za 
Kitanzania.

Mmoja ya 
wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 
akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB 
ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).

Safari ya
 kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa 
wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa 
kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. (J.G)




Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini.

Kazi ya 
kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo 
washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48.

Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo.
No comments:
Post a Comment