Alichoamua kufanya Messi baada ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Barca
Jumamosi
iliyopita, Lionel Messi aliweka rekodi nyingine kubwa kwenye soka,
dhidi ya Osasuna aliifikia na kuipita rekodi ya magoli ya gwji wa klabu
ya FC Barcelona Paulino Alcantara, ambaye aliifungia Barca jumla ya
mabao 369.
Messi aliivunja rekodi hiyo kwa kufikisha mabao 371, baada ya kupiga
hat trick dhidi ya Osasuna, na katika kusherehekea rekodi hiyo – Messi
aliamua kuvaa jezi ya Paulinho Alcantara pamoja na mpira – vifaa vya
michezo ambavyo Alcantara alivitumia miaka ya 1920s.
No comments:
Post a Comment