CRIMEA YATANGAZA RASMI KUWA SEHEMU YA SHIRIKISHO LA RUSSIA
Wanawake wa Crimea wakiwa Simferopol, Ukraine wakifurahia kujitenga kwao kutoka Ukraine na kuwa sehemu ya Russia
Maafisa katika Jamhuri ya Crimea
iliyojitenga na Ukraine wanasema wapiga kura kwa idadi kubwa
wameidhinisha kujiunga na Russia katika kura ya maoni iliyokuwa na utata
ambayo imefanya viongozi wa magharibi kujiandaa na vikwazo dhidi ya
Moscow. Jumatatu bunge la Crimea liliidhinisha kura ya maoni, kutangaza
uhuru na kuwa rasmi sehemu ya Russia.
Hivi sasa imetangazwa rasmi wa-Crimea
tayari wapo chini ya udhibiti wa Russia na wanaiunga mkono Russia
wamefanya uchaguzi wa kujitenga kutoka Ukraine na kuungana na Russia.
Kufuatia kura ya jumapili ya kujiunga na Russia, bunge la kieneo la
Crimea limeomba kuwa sehemu ya shirikisho la Russia.
Lakini nini kinachofuata baada ya kura
ya maoni, wote viongozi kwenye peninsula ya Black Sea na dunia
waligawanyika katika njia ambazo zinakumbusha mivutano ya enzi ya vita
baridi, viko mbali kumalizika.
Wabunge huko Moscow wanaahidi kuweka
kando vikwazo vya kisheria ili kuiruhusu Crimea kuingia kwenye
shirikisho la Russia. Lakini wasi wasi wa haraka kwa eneo ambalo halina
mpaka wa ardhi na Russia unajumuisha usambazaji wake wa nishati, maji na
bidhaa nyingine za msingi ambazo hivi sasa wanayapata kutoka Ukraine.
Moscow inatetea hatua ya Crimea kama
kuongeza kanuni za kujitambua wenyewe. Mazungumzo kwa njia ya simu kati
ya Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Russia Vladimir Putin
yanaripotiwa kuleta mafanikio kidogo kuziba mwanya uliopo.
Waangalizi wa kigeni walioalikwa na
Crimea inayoungwa mkono na serikali ya Russia walitetea kura ya maoni
kama inaendeleza kanuni za kimataifa. Mwangalizi kutoka Ubelgiji, Frank
Creyelman aliwapuuza wakosoaji wakiwemo kutoka serikali mpya huko Kyiv
kwamba upigaji kura ulifanyika kwa mtutu wa bunduki.
Chanzo, voaswahili (R.M)
No comments:
Post a Comment