Ratiba ya Mkutano wa bunge maalum imetoka kuanzia leo Tar 17- 21 March
Ofisi
ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma
kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dodoma leo kwa
ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.
Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum
wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum leo saa 2:00
asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge
Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge
Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa
semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa
Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi
rasmi wa Bunge Maalum Atakaye ipata taarifa hii amjulishe mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya KATIBU WA BUNGE
No comments:
Post a Comment