Huu uharibifu uwanja wa taifa umeleta hasara ya milioni 15, soma kilichosemwa na serikali.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo kupitia afisa habari wao Wambura
wametoa ya moyoni kuhusu uharibifu unaofanywa na shabiki wa timu
mbalimbali >> ‘tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali
unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile
za kimataifa na ligi za hapa nchini’
‘Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye
mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya
Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam’
Taarifa
inasema Uharibifu wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa
wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali na TFF imesema italipa fedha
hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
‘Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa
klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali
ili iwe fundisho kwa wengine’
Kwa mujibu wa Serikali viti kumi vimeng’olewa na kutupwa ovyo ovyo
uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji
waliokuwepo.
‘Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye
dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya
kutumia uwanja huo’
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki,wapenzi na wanachama wa klabu
mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na
mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika
endapo kutatokea uharibifu.
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi na
kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi..
No comments:
Post a Comment