Kauli ya M/kiti kutokana na bunge kuahirishwa baada ya malumbano ya Ole Sendeka na Waziri Hamis
Kwenye bunge maalum la katiba Alhamisi ya March 6 2014 Dodoma, mwenyekiti wa Muda wa Bunge Pandu Ameir Kificho alilazimika kuahirisha semina ya bunge maalum kutokana na kutokea vurugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe, kupinga kitendo cha kiti cha mwenyekiti kupendelea baadhi ya wabunge.
Vurugu
 hizo zilianzia pale waziri wa sheria wa Zanzibar ambae pia ni mjumbe wa
 kamati ya kanuni ABOUBAKAR HAMIS BAKARI alipolalamikia kitendo cha 
baadhi ya wajumbe kuwasilisha mabadiliko ya kanuni, licha ya majina yao 
kutopitishwa kwenye kamati ya kanuni ili mapendekezo yao yajadiliwe.
Baada
 ya hayo, Mbunge wa Simanjiro CHRISTOPHER OLE SENDEKA, ambae ni mmoja wa
 wajumbe wanaodaiwa kupendelewa alibainisha kwa kuwasilisha mapendekezo 
yake kwa wakati kwa kusema  
‘Na
 mimi sio dhaifu kwa kanuni na taratibu zinazoongoza mabunge, kazi yetu 
sio kupeleka marekebisho yetu kwa Aboubakar, kama Aboubakar ana chama 
chake hoja zangu zinamuuma asimame na kudeclare interest’ 
Kauli hiyo ilimfanya Aboubakar kuwasha kipaza sauti na kusema
 ‘Kuanzia mwaka 1980 niko kwenye haya Mabunge, ni miaka 34…… sifikirii 
kama mtu katoka Simanjiro miaka kumi iliyopita akaja hapa akasema anajua
 kanuni, sitaki kuombwa radhi lakini ajue kwamba kuna watu wanaojua 
zaidi kuliko yeye’
Malumbano
 haya ndio yalifanya Mwenyekiti kuchukua hatua muda huohuo kwa 
kuliahirisha bunge mpaka jioni ambapo liliendelea na shughuli zake kama 
kawaida japo baada tu ya kurejea, Mwenyekiti alisema 
 ‘Wale ambao tuliwapa kazi ya kuonana na Waheshimiwa Bakari na Ole 
Sendeka wameniletea taarifa nzuri kwamba kimsingi wawili hawa 
wamekubaliana na jambo lile limekwisha, nawashukuru sana hawa 
Waheshimiwa wangu kwa kulimaliza kwa mioyo kunjufu sana na kupata 
taarifa kwamba kila mmoja wao hana kinyongo chochote dhidi ya mwenziwe’
Nae James Mbatia alisema 
 ‘tumezungumza na tunamshukuru sana ndugu yetu Waziri wa sheria wa 
Zanzibar Aboubakar Hamis na kaka yangu Christopher Ole Sendeka kuweza 
kuridhiana na kuona ni changamoto tu imetokea na sasa kuwa wamoja, sisi 
sote ni watu wazima na tuko hapa kwa niaba ya Watanzania na kila mmoja 
wetu anabeba roho za Watanzania elfu sabini na mia nne’
No comments:
Post a Comment