WAHAMIAJI HARAMU 40 WAZAMA YEMEN

Maafisa wa serikali nchini Yemen 
wamesema kuwa zaidi ya wahamiaji arubaini wa Kiafrika wamezama baharini,
 baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama, katika pwani ya kusini 
mwa nchi hiyo.
Manuwari ya jeshi la Yemen ambalo lilikuwa katika eneo hilo, imefanikiwa kuwaokoa wahamiaji wengine wapatao thelathini.
Wizara ya ulinzi nchini Yemen imesema 
kuwa mashua hiyo iliyokuwa ikisafirisha wahamiaji haramu, ilizama katika
 mkoa wa Kusini wa Shabwa, eneo ambako maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika 
huwasili kila mwaka.
Kwa 
mujibu wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji la IOM, wengi wa wakimbizi 
wanaojaribu kuvuka guba la Eden, wanatoka Somalia na Ethiopia.
Shirika hilo limesema kuwa wahamiaji 
hao hufanya safari ndefu na hatari ili kukwepa umasikini, unyanyazaji au
 vita katika mataifa yao.
Baada ya kuwasili Yemen, wengi wao 
hutarajia kupata kazi nchini Saudi Arabia na mataifa ya Guba, lakini 
mamia ya wahamiaji wa Kiafrika hufa kila mwaka wakijaribu kuvuka eneo 
hilo la Guba wakitafuta maisha bora katika mataifa ya ngambo.(P.T)
No comments:
Post a Comment