JICA WAJIPANGA KUIPIGA TAFU TANZANIA KWA UJENZI WA DARAJA
SHIRIKA lisilo la kiserikali toka Nchini Japan , JICA ALUMNI
ASSOCIATION OF TANZANIA (JATA)
imejipanga kwa mwaka huu kusimamia miradi mikubwa miwili kwa mwaka
2014/2015 itakayofadhiliwa na Serikali ya Japan
hapa nchini.
Miradi hiyo imetajwa kuwa ni ujenzi wa daraja la juu ,
litakalojengwa eneo la Tazara na maendeleo ya elimu katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Hayo yalisemwa na Mwakilishi Mkuu wa JICA Bw. Yasunori Onishi , wakati akifungua mkutano wa
mwaka wa JATA , ambapo alisema kuwa kwa
sasa Tanzania na Japani imejenga
mahusiano mazuri na raia wao wengi wapo nchini kwa ajili ya kufanya
biashara na kutekeleza miradi ya
maendeleo.
Bw. Onishi alisema Serikali ya Japani inampango wa
kutekeleza miradi hiyo mikubwa miwili ndani ya mwaka 2014/2015 kwa lengo la
kuboresha mahusiano zaidi juu ya
kuwawezesha vijana wengi kupata elimu ya viwanda ili wajijengee uwezo wa kujiajiri .
“ Mbali na hilo lazima tuwekeze pia kwenye miumdo mbinu kama
kujenga hilo daraja la juu ambapo itasaidia kupunguza msongamano wa foleni
za magari ambapo kwa sasa ni kero kubwa
jijini na daraja hilo litajengwa eneo la Tazara” alisema Bw. Onishi
Alisema mbali na miradi hiyo ambayo imepangwa kutekelezwa
, Japani kwa kupitia JICA imekwisha tekeleza miradi mbali mbali nchini kama kukabiliana na utatuzi wa tatizo la maji na umeme
katika visiwa vya Unguja na Pemba , kusimamia maswala ya mazingira,
kusimamia miradi mikubwa ya maji katika
mto wa Wami Dakawa.
Aliendelea kueleza kuwa mambo mengine waliyofanya ni kuibua ushindani wa wanadunzi wa shule za
sekondari katika kuandisha insha na kuwapatia zawadi , Kutembelea na kutoa
ushauri wa kitaalamu katika chuo cha teknolojia
kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Miradi ya kilimo cha umwagiliaji , mradi wa
kutengeneza vyombo vya udongo , Pamoja na mradi wa ufuatiliaji wa mipango
mikakati katika maendeleo ya majimbo
Zanzibar.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa JATA nchini Bw. Omar Kassim Omar alisema Serikali
ya Japani kwa kupitia shirika lao hilo, imekuwa ikifadhili na kuendelea
kufadhili shughuli mbalimbali za
maendeleo hapa nchini , ambapo wameona zikiwa katika mafanikio makubwa hasa kwenye upande wa kutoa elimu kwa vijana,
kwani wapo baadhi ya wajapani wamekuwa wakitoa mafunzo katika shule za sekondari
ya sayansi na hisabati bure.
Alisema JATA imepanga
kuibua miradi mbali mbali ikiwemo ya afya, mazingira, elimu, kuendesha semina
kwa vijana na mambo mengine ambazo
zitasimamiwa vema na kufadhiliwa na Japan.
Mbali na hayo JATA pia ilifanya uchaguzi wa viongozi wapya
watakao simamia vema utekelezaji wa miradi iliyopangwa kufanyika ambapo nafasi
ya Mwenyekiti ilishikwa na Bw. Twaha
Twaha , Makamu Mwenyekiti ni Bw. Omar Kassim Omar, Katibu ni Edna Ngeregeza na katibu Msaidizi ni Bw. Perer Mtaita na mweka hazina ni Zuhura
Mwakijinja.
Wajumbe wengine wanaounda kamati ni Kassimu Shaali , Jacob Kattanga, Milton
Rwegasira na Mudrick Fadhili Abasi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment