TAIFA STARS KUTUMIA JEZI ZA ADIDAS

Hizi ndiyo Jezi mpya za Adidas za Taifa Stars
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 
(TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Kufuatia makubaliano hayo TFF 
tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa
 (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye 
mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini 
Windhoek.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas 
ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu 
(FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu 
nchini.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF) (P.T)
No comments:
Post a Comment