Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya kufungwa na Barca hiki hapa
Cristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza Barca yenye wachezaji 12.
Mwanasoka huyo bora wa dunia amesema kwamba refa wa mchezo huo 
Undiano Mallenco alichangia timu yake kupoteza wa El Clasico hapo jana 
usiku katika dimba la Santiago Bernabeu.
Madrid walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili 
kuanza, lakini Mallenco aliwapa Barca penati mbili muda mfupi baadae — 
pia alimtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos – na Ronaldo anasema anahisi 
refa alikuwa akiwapendelea Barcelona kwa makusudi.
“Undiano Mallenco hafai kuchezesha michezo ya namna hii. Tulikuwa 
tunacheza dhidi ya wachezaji 11 na mwingine wa ziada. Mara zote imekuwa 
hivi. Ni kama vile hawataki tushinde ili Barca watetee taji la La Liga,”
 Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari.
“Sitafuti visingizio, lakini sitaki kukaa kimya kuhusu hili. Refa huyu hakustahili kuchezesha mchezo wa namna hii.
“Nimekuwa hapa kwa muda mrefu – miaka mitano, nafahamu mambo 
yanavyoenda. Kama Barcelona wangepoteza mchezo hu, wasingekuwa na 
matumaini ya ubingwa tena. Sijawahi kuona Madrid wakipendelewa na refa.”
“Pamoja na yote yaliyotokea, Madrid bado tutachukua ubingwa wa La Liga.”
No comments:
Post a Comment