UCHUNGUZI WA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOTOTOWEKA WAENDELEA

Waziri wa
 uchukuzi wa Malaysia anasema uchunguzi umeanza kubaini utambulisho wa 
abiria wanne waliokuwa ndani ya ndege ya Malaysia iliyotoweka, ambao 
walikuwa na pasi za kuiba na stakabadhi nyingine bandia.
Waziri 
huyo wa uchukuzi Hishammuddin Hussein aliwaambia waandishi habari 
Jumapili kuwa idara za kijasusi za Malaysia zinapeleleza orodha ya 
abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo na kushirikiana na wenzao wa 
kimataifa ikiwemo idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya Marekani FBI.
Maafisa 
wanasema pia kuwa kifaa cha ufuatiliaji wa safari za ndege kinaashiria 
ndege hiyo ilirudi nyuma badala ya kuendelea na safari yake kabla ya 
kutoweka. Timu za uokozi bado zinaendelea na juhudi za kuitafuta ndege 
hiyo.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment