MKUU WA JESHI KUGOMBEA URAIS MISRI
Mkuu wa
majeshi na waziri wa ulinzi Misri, Abdul Fattah al-Sisi, ametangaza
kujiuzulu jeshini ili kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao.
Wagombea wote wanapaswa kuwa raia.
Akizungumza
Kwenye hotuba ya Televisheni huku akiwa amevalia sare ya kijeshi Abdel
Fattah El Sissi amesema yeye sio mwanajeshi tena baada ya miaka 44 na
kwamba amechukua hatua hiyo ili aweze kutimiza jukumu lingine muhimu.
Ni Bayana kwana Sisi hatakua na
kibarua kigumu kujipatia ushindi katika uchaguzi wa Urais. Anaungwa
mkono na idadi kubwa ya raia wa Misri na hadi sasa hana wapinzani
wowote.
Baadhi ya waliotaka kugombea urais wamejiondoa wakidai kwamba hawataweza kuendesha kampeni zao kwa njia huru.
Wafuasi wake Sisi wanamuona kama
kiongozi imara ambaye anaweza kurejesha amani na udhabiti nchini Misri
baada ya miaka mingi ya machafuko.
Wakosoaji wake wanasema ana msimamo mkali na amechangia pakubwa katika kusambaratisha na kuhujumu upinzani nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi atakabiliwa na
majukumu mazito ya kufufua uchumi uliofifia , kupambana na uasi na
kuileta pamoja nchi iliyogawanyika. Ameahidi kutekeleza mabadiliko
makubwa lakini akaonya kuwa hawezi kufanya miujiza.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment