MANCHESTER CITY YATUPWA NJE KOMBE LA FA

wachezaji wa timu ya Wigani wakimpongeza Jodri Gomez baada ya kupachika goli kwa njia ya mkwaju wa penati.
Na Riziki Mashaka.
Timu ya Wigan imeichapa Man City 
magoli 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Etihad katika hatua 
ya robo fainali ya kombe la FA.
Jodri Gomez aliindikia Wigan goli la 
kwanza kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 27, wakati James Perch 
alipachika goli la pili katika dakika ya 34 na kuiwezesha timu hiyo 
kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 mpaka timu hizo zikienda mapumziko, 
Samir Nasri alipiga msumari wa moto na kumwacha mlinda mlango wa Wigan 
akishangaa na kuiwezesha timu hiyo kulipa goli 1 lakini mpaka mwisho wa 
mchezo, Man City ilijikuta ikiondolewa katika mtanange huonkwa jumla ya 
magoli 2-1.
Matokeo ya mchezo huo yameifanya timu 
ya Man City kutolewa katika kinyang'anyiro cha kombe hilo, itakumbukwa 
kuwa Man City walitolewa na Wigan katika fainali za kombe la FA mwaka 
jana, hivyo kichapo cha leo ni pigo jingine kwa timu hiyo ambayo siku 
chache zijazo itakumbana na Barcelona katika mchezo wa raundi ya pili ya
 kombe la klabu bingwa ya ulaya.
No comments:
Post a Comment