Vitu vinavyoelea Bahari ya Hindi huenda vikawa mabaki ya ndege ya Malaysia

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott 
ameliambia bunge kwamba picha za setaliti zinaonesha vifaa vinavyo 
fanana na mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea nje ya pwani ya kusini 
magharibi ya Australia katika eneo kusini ya Bahari ya HIndi.
Bw. Abbott anasema ndege ya kijeshi 
imepelekwa katika eneo hilo na inatazamiwa kuwasili Alhamisi mchana saa 
za Austrlia, na ndege nyingine tatu zitapelekwa kuanza uchunguzi wa kina
 kutafuta eneo hilo.
Hata hivyo Bw Abbot alionya kwamba 
kazi za kutafuta na kupata vyombo hivyo inaweza kua ngumu na huwenda 
visihusiane na ndege hiyo nambari MH370.
Voaswahili (R.M)
No comments:
Post a Comment