MAANDAMANO YASHTADI UKRAINE KUIPINGA SERIKALI HIYO
Miji ya
kusini na mashariki nchini Ukraine imekuwa uwanja wa maandamano makubwa
ya wananchi dhidi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo. Maelfu ya
wananchi katika miji ya Donetsk, Kharkiv, Odessa na miji mingine ya
kusini na mashariki mwa nchi hiyo, walimiminika mabarabarani hapo jana
wakipinga mwenendo wa viongozi wa serikali ya Kiev. Kwa mujibu wa
ripoti, waandamanaji wametaka nao kuitishwa kura ya maoni kwa ajili ya
kujitenga na kujiunga na shirikisho la Russia kama lilivyofanya hivi
karibuni jimbo la Crimea sanjari na kurejeshwa madarakani Viktor
Yanukovych kama Rais wa halali aliyechaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
Kwa upande mwingine, maelfu ya wananchi wamejitokeza mjini Kiev, mji
mkuu wa Ukraine wakiunga mkono viongozi wa sasa na kutaka kudumishwa
umoja wa kitaifa nchini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo suala la
kujitenga eneo la Crimea kutoka Ukraine na kujiunga na Russia
limeendelea kushadidisha uadui kati ya Moscow na nchi za Magharibi.
(J.G)
No comments:
Post a Comment