KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA AELEKEA MOSCOW NA KYIEV
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki
Moon yuko njiani kuelekea Moscow na Kyiev katika juhudi za kusaidia
kutafuta suluhu la kidiplomasia kwa mzozo wa Peninsula ya Crimea.
Ofisi ya Bw.Ban imeeleza kwamba
atawasili katika mji mkuu wa Russia Alhamisi na kukutana na rais Vladmir
Putin. Na Pia atafanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje Sergei
Lavrov na maafisa wengine wa juu .
Ijumaa ataelekea Ukraine ambako
atakutana na rais wa mpito Oleksandr Turchymov na waziri mkuu wa muda
Arseniy Yatsenyuk na pia maafisa wengine waandamizi.
Msemaji wa Umoja wa mataifa Farhan Haq
alirudia kueleza kwamba katibu mkuu alikuwa akitarajia kupatikana
suluhisho la kidiplomasia kwa suala hilo.
Siku ya Jumapili eneo la Crimea la
Ukraine lilifanya kura ya maoni ya haraka kukiwepo maelfu ya wanajeshi
wa Russia na kupiga kura ya kujitenga na Ukraine wakiwa na nia ya
kujiunga na muungano wa Russia.Viongozi wa muda wa Ukraine wametangaza
kura hiyo ni kinyume cha sheria chini ya katiba ya nchi hiyo.
Wakati wa ziara yake fupi katibu mkuu
pia atakutana na wanachama wa tume ya wafuatiliaji wa umoja wa mataifa
wakati akiwa Kyiv. Umoja wa mataifa umeomba kupeleka wasimamizi huko
Crimea ili kutathmini hali ilivyo.
Chanzo, voaswahili (R.M)
No comments:
Post a Comment