Inavyoendelea hali ya kiafya ya Michel Schumacher baada ya ajali mbaya
 
Bingwa
 wa zamani wa mashindano ya Fomula 1 Michael Schumacher, amekuwa 
akionyesha dalili nzuri baada ya madaktari kuanza kumtoa katika hali 
yake mahututi.
Familia yake imesema kuwa bado ina matumaini kwamba Michael ataweza kuamka.
Madaktari nchini Ufaransa wamekuwa wakifanya juhudi za kumuamsha 
Michael ambaye ni bingwa mara saba wa Formula 1 kutoka katika hali yake 
ya kupoteza fahamu.
Schumacher mwenye umri wa miaka 45 kutoka Ujerumani, alipata majeraha
 mabaya ya kichwa alipokuwa anashiriki mchezo wa kuteleza kwa barafu 
mwezi Disemba 29 katika maeneo ya Alps Ufaransa.
Madaktari walimuweka Schumacher katika hali ya kupoteza fahamu ili kuzuia uvimbe katika ubongo wake.
Familia ya Schumacher imezungumza na kusifu jitihada za madaktari wa 
Ufaransa na pia wamesema kuwa hiki ni kipindi kigumu kwao na kuwa hawana
 budi ila kuwa na subira.
Wachunguzi wanasema kuwa Schumacher hakuwa anaenda kwa kasi kubwa wakati wa ajali hiyo ingawa alianguka alipokuwa akiteleza.
Schumacher alistaafu kutoka katika mashindano ya Formula 1 mwaka 2012 baada ya kushiriki mwa miaka 19.
Alishinda mataji mawili akiwa na kampuni ya Benetton mwaka 1994 na 
1995,kabla ya kuhamia kampuni ya Ferrari mwaka 1996 na kuendelea 
kushinda mataji mengine matano kuanzia mwaka 2000.
No comments:
Post a Comment