Van Vicker aingia Tanzania kuigiza bongomovie, Hashimu Kambi aelezea kuhusu movie hiyo

Van Vicker muigizaji kutoka Ghana ambaye anafanya vizuri hadi nchini 
Nigeria ameingia Tanzania jumapili iliyopita na anaondoka leo tarehe 
19/9 kurudi kwao Ghana. Hashimu Kambi ambaye ndiyo mwenyeji wake 
akiongea na millardayo.com alisema,”Van Vicker amekuja Tanzania kuigiza 
movie yangu ambayo mwanzoni niliipa jina la
 The Network. Lakini kutokana na kuwa kuna movie nyingine ambayo imetoka
 na jina hilo hilo nimeamua ku-change jina. Hadi sasa nina majina manne 
bado sijaamua kutumia lipi.”
Hashimu Kambi aliendelea,”Vicker amefika hapa Tanzania jumapili na 
anamalizia baadhi ya scene leo na ataondoka leo usiku tare 19/9. Kazi 
ikiwa tayari tutawaambia inavyotoka na watanzania wasubili kitu kizuri 
kwasababu kwenye hii movie kuna watu kama Vicker mwenyewe,Weru 
Sengo,Irene Paul na wengine. So, itakuwa kazi nzuri sana”
Van vicker  anaonekana kufurahia kuwa Tanzania kwasababu amekuwa akipiga picha sehemu nyingi sana anazokuwa.


![]()  | 
| Van na Lulu | 

No comments:
Post a Comment