DK. NCHIMBI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani iliyozinduliwa Kitaifa jijini Mwanza leo. Wa pili kulia ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza
Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Mohamed Mpinga. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA
SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Washiriki
wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya
kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika
Uwanja wa Mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo. Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi aliyazindua maonesho hayo huku
akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani
ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Polisi
kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Dumu Mwalugenge, akitoa
maelezo kwa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi (kushoto), namna ajali barabarani zinaweza kuepukika endapo
watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani.
Waziri Nchimbi aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani katika Kiwanja cha Mpira CCM Kirumba jijini Mwanza leo. Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA
MIMI, WEWE NA SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.(hd)
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiwa amevaa jaketi pamoja
na kofia ngumu ambapo mavazi hayo huwa yanavaliwa wakati ya uzimaji wa
moto. Waziri Nchimbi alivaa mavazi hayo wakati alipokuwa ndani ya banda
la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika maonyesho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani ambayo aliyazindua jijini Mwanza leo. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA
SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la
Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima kwa mchango wake aliouonesha
katika kusimamia mapambano ya kutokomeza ajali za barabarani nchini.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA
MIMI, WEWE NA SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waendesha pikipiki (bodaboda) na baiskeli nao pia walishiriki
kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja
cha Mpira cha CCM Kirumba, jijini Mwanza leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho
ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI
SOTE"Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (watano kutoka kushoto),
Naibu Waziri wa wizara hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama
Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati) pamoja na maafisa usalama
barabarani na wadau wa usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
ambayo Kitaifa yamezinduliwa na Waziri Nchimbi, jijini Mwanza leo. Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA
MIMI, WEWE NA SISI SOTE". Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment