MAN UNITED YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 KOMBE LA LIGI

Javier Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao pekee la Manchester United Uwanja wa Old Trafford

MACHO yote yalikuwa kwa Luis Suarez 
baada ya kurejea Liverpool kufuatia kumaliza adhabu yake ya mechi 10, 
lakini Javier Hernandez akaiteka shoo kwa bao lake pekee lililoipeleka 
Manchester United Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital 
One.Hatimaye Suarez alicheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya baada ya
 kumaliza kutumikia adhabu yake ya kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav 
Ivanovic msimu uliopita.(P.T)
Na wakati mshambuliaji huyo wa Uruguay
 alizomewa na mashabiki Uwanja wa Old Trafford, alikuwa ni Chicharito 
aliyepoza maumivu ya David Moyes kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka 
kwa wapinzani, Manchester City katika Ligi Kuu Jumapili.
Liverpool ilitawa sehemu kubwa ya 
mchezo na Daniel Sturridge alipoteza nafasi kadhaa nzu za kufunga, 
lakini Hernandez hakufanya makosa alipopata nafasi dakika ya 46.
Wayne Rooney, ambaye ndiye mchezaji 
bora zaidi kwa United hivi sasa, alipiga kona nzuri baada ya mapumziko 
na Hernandez akaunganisha nyavuni.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez.
Liverpool: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez na Moses, Sturridge.
No comments:
Post a Comment