TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, September 24, 2013

MJUMBE WA UN SOMALIA : Al-SHABAAB WATOKOMEZWE

somali 2d4a5
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametaka kuzidishwe mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la ash-Shabab. (HM)
Nicholas Kay ameyasema hayo jana
katika kikao na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswis na kuitaka jamii ya kimataifa izidishe juhudi za kupambana na kundi hilo. Amesema kuwa hadi sasa serikali ya Somalia imeweza kwa kiasi fulani kurejesha hali ya usalama katika maeneo mengi ya nchi hiyo na akaongeza kuwa, pamoja na hayo bado kuna haja ya kuisaidia nchi hiyo kwani serikali ya Mogadishu bado inakabiliwa na kundi hilo.
Kay amesema shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa al Shabab dhidi ya jengo la kibiashara huko mjini Nairobi, Kenya sio la kushangaza, kwani ni miongoni mwa jinai kubwa ambazo zimekuwa zikitekelezwa na kundi hilo. Amesema kuwa, usalama wa Somalia unategemea kusambaratisha kwa kundi hilo la ash-Shabab.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon ameiomba jamii ya kimataifa kusaidia juhudi za kuliangamiza kundi la kigaidi la al Shabab ambalo limetangaza kwua ndilo lililotekeleza shambulizi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi.
CHANZO: RADIO TEHRAN

No comments:

Post a Comment