TPA YASHIRIKI SIKU YA BAHARI DUNIANI
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akizungumza na
wadau(hawapopichani) wanaohusika na sekta ya usafirishaji majini wakati
wa kongamano la kuadhimisha siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini
Mwanza hivi karibuni.
Naibu
Waziriwa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa sekta ya usafirishaji majini wakati wa kongamano la kuadhimisha
siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
TPA yaadhimisha siku ya Siku ya Bahari Duniani
Na Focus Mauki
Afisa Mawasiliano-TPA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) imeshiriki maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani
yaliyofanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North.
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Bahari Duniani (IMO) linaadhimisha Siku ya Bahari Duniani, Septemba 26 kila mwaka.
Maadhimisho hayo hufanyika mara moja
kila mwaka ambapo pamoja na mambo mengine Jumuiya ya Kimataifa ya Bahari
ikiongozwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO), huyaadhimisha kwa
kutathimini usimamiaji wa ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira
baharini na katika maziwa.
Tanzania ikiwamo nchi nyingine
wanachama wa IMO huadhimisha siku hii kwa kufanya maonyesho ya siku
mbili ambayo huandaliwa na SUMATRA. Kwa mwaka huu maonyesho haya
yamefanyika Septemba 25 na kufikia kilele chake Septemba 26 mwaka huu.
Pamoja na kuwa na maonyesho kwa umma,
SUMATRA iliandaa kongamano lililofanyika Septemba 26 ambalo lililenga
kuonyesha mchango wa Sekta ya Bahari na Bandari katika kukuza na kuleta
maendeleo endelevu hapa nchini.
Kaulimbiu katika maadhimisho ya mwaka
huu ni, 'Maendeleo endelevu: Mchango wa IMO kupitia Agenda ya Rio +20'.
Kwa mujibu wa SUMATRA kauli mbiu ya mwaka huu imechaguliwa kuonyesha
mchango wa IMO kwa mwaka 2013 katika kubeba jukumu la kutekeleza
makubaliano ya kimataifa juu ya kuleta maendeleo endelevu yaliyoafikiwa
katika kikao kilichofanyika Juni 20 hadi 22, 2012, Rio de Janeiro,
Brazil kijulikanacho kama 'Rio+20'.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA,
Alhaj Ahmad Kilima amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Umoja wa
Mataifa umechukua hatua za kimaendeleo kwa kuweka malengo mengi ili
kufikia maendeleo endelevu ambayo hayatoathiri uwezo wa dunia, mfumo
asilia pamoja na kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili
jamii.
Sekta ya bahari ina mchango mkubwa
katika mihimili mitatu ya maendeleo endelevu ambayo ni uchumi, jamii na
utunzaji wa mazingira ya bahari. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha Bandari
zake kote nchini, ili imeweka mazingira na miundombinu ya kisasa
itakayotoa mchango katika kufikia malengo yaliyopo kitaifa na kimataifa
No comments:
Post a Comment