TARIBO WEST, KESHI WAPORWA MALI
SUPASTAA wa zamani wa Nigeria, Taribo
West na kocha wa sasa timu ya taifa ya nchi hiyo, Stephen Keshi,
wameripotiwa kuporwa ardhi waliyopewa kama zawadi baada ya kuisaidia
Super Eagles kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2002 zilizofanyika Japan
na Korea Kusini. (HM)
Wawili hao sambamba na wachezaji
wengine waliokuwa wakiunda Super Eagles waligawiwa vipande vya ardhi
katika eneo la Port Harcourt, kusini mwa Nigeria na gavana wa zamani wa
Rivers State, Peter Odili.
Hata hivyo, kwa mujibu wa West maeneo
hayo yameporwa na wavamizi na aligundua hilo baada ya kwenda kwenye
ardhi yake akitaka kuanza kuiendeleza.
"Nilikwenda kwenye eneo langu na
kukuta limechukuliwa na wavamizi. Si mimi pekee, kuna wachezaji wengi
akiwamo Keshi maeneo yao yamechukuliwa pia," alisema West huku
akionyesha kuchukizwa na jambo hilo. West alichezea Nigeria mechi 41
kati ya 1994 na 2002. Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment