ICC YAMRUHUSU WILLIAM RUTO KUREJEA KENYA
Bwana Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 nchini kenya.
Ruto na Rais Uhuru Kenyatta,
wanakabiliwa na tuhuma za za uhalifu dhidi ya binadamu baada ya kudaiwa
kuhusika na ghasia za kikabila baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008
ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
Mahakama iliakhirisha kesi baada ya
kikao cha dharura kuitishwa huku upande wa mashtaka ukisema kuwa hauna
pingamizi lolote ikiwa kesi zitaakhirishwa kwa muda mfupi.
Mwakilishi mmoja wa mashahidi aliangua
kilio mahakamani na kutaka mahakama iweze kumruhusu Ruto kurejea
nyumbani kushughulikia swala hilo la dharura.
''Kutokana na hali ilivyo na maoni
tuliyoyasikia , mahakama inamruhusu Ruto kurejea nyumbani kwa muda wa
wiki moja,'' alisema jaji anayesimamia kesi hiyo, Chile Eboe-Osuji.
"Kwa sasa Ruto ataruhusiwa kusalia Kenya kwa wiki moja, ila ikiwa atatoa ombi lengine,'' alisema jaji Chile.
Kwa mujibu wa wakili wa Ruto,Karim
Khan, alitarajiwa kuondoka Uholanzi saa tatu asubuhi, saa za Afrika
Mashariki. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment