MAN UNITED YAUA 4-2 ULAYA, ROONEY APIGA 2
Wayne Rooney Akifunga bao (HM)
KOCHA David Moyes ameonyesha nini
alihitaji kucheza soka ya wazi, soka adimu Uwanja wa Old Trafford,
ambayo matunda yake ni kushinda mabao mengi, 4-2 dhidi ya Bayer
Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi Ligi
ya Mabingwa usiku wa kuamkia leo.
Hadi sasa, Moyes wakati wote amekuwa
akijaribu kuwatumia pamoja Robin van Persie na Wayne Rooney pale mbele.
Sasa wako upande wake na wanamfanyia kazi nzuri.
Van Persie amefunga moja ya mabao ya
msimu, Rooney amefunga mawili na lingine Antonio Valencia katika ushindi
ho na sasa wanaelekea kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao, Manchester
City wakiwa wenye kujiamini.
Faraja kwa Rooney leo ametimiza mabao
200 ya kuifungia United, hivyo kuingia kwenye orodha ya magwiji wa
klabu, Bobby Chartlon mabao 249, Dennis Law 237 na Jack Rowley 211.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Damir Skomina wa Slovenia, Rooney alifunga dakika ya 22 na Bayer wakasawazisha kupitia kwa Rolfes dakika ya 54, kabla ya Van Persie kufunga la pili dakika ya 59, Rooney tena la tatu dakika ya 70 na Valencia dakika ya 79 kabka ya wageni kupata bao la pili dakika ya 88 kupitia kwa Toprak.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Damir Skomina wa Slovenia, Rooney alifunga dakika ya 22 na Bayer wakasawazisha kupitia kwa Rolfes dakika ya 54, kabla ya Van Persie kufunga la pili dakika ya 59, Rooney tena la tatu dakika ya 70 na Valencia dakika ya 79 kabka ya wageni kupata bao la pili dakika ya 88 kupitia kwa Toprak.
Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea,
Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Fellaini/Cleverley
dk81, Kagawa/Young dk71, Rooney/Hernandez dk84 na Van Persie.
Bayer Leverkusen: Leno, Donati,
Spahic, Toprak, Boenisch, Can, Reinartz, Rolfes, Sam/Kruse dk78,
Kiessling/Derdiyok dk78 na Son/Benderdk 64.Uteuzi wa timu wa Moyes
unamaanisha Ryan Giggs atasubiri sana kuongeza idadi ya mabao yake.
Mkongwe huyo wa United, akiwa
amebakiza miezi miwili kusherehekea kutimiza miaka 40, amefungana kwa na
gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul katika kucheza mechi nyingi katika
Ligi ya Mabingwa, wote 144).
Na kwa kuwa Giggs hakuwepo hata
benchi, kuna uwezaekano ikamchukua muda sana. Giggs na Raul wanafuatiwa
na Paolo Maldini (mechi 140), Xavi (mechi 136), Clarence Seedorf (mechi
131), Paul Scholes (mechi 130) na Iker Casillas (mechi 129). Chanzo:
binzubeiry
No comments:
Post a Comment