MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL
CHIFU wa Arsenal, Stan Kroenke anataka
kocha Arsene Wenger abaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na kuleta
taji la Ligi Kuu ya Enland Emirates. (HM)
Mfaransa huyo amekuwa katika klabu
hiyo kwa miaka 17 na The Gunners ikiwa inakabiliwa na ukame wa mataji
kwa msimu wa tisa sasa, amekuwa akipigwa zengwe aondoke, hususan
kutokana na Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.
Lakini mtu mwenye hisa nyingi za klabu, Kroenke hana shaka anataka Wenger abaki.
Mmarekani huyo amesema kwamba hafikiri kama kuna mwingine bora kuliko yeye na anaamini Wenger anafanya kazi nzuri.
Alipoulizwa kama mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 yumo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, Kroenke alisema: "Hiyo ni sahihi kabisa. Arsene anafahamu ambavyo tunahisi, falsafa zetu ni nini, nini tunataka kufanya na ninahisi tuko pamoja sana,".
Kufuatia klabu kuvuna rekodi yake ya usajili kwa kumsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid.
Kroenke alisema: "Kwa kweli namfurahia Arsene - safi sana, mweledi. Ana upeo mkubwa wa uongoza timu na klabu. Yuko sahihi katika hilio.
Kroenke pia amesema Wenger hastahili lawama kwa klabu hiyo la Kaskazin mwa London kumkosa mshambuliaji Luis Suarez, kwani ni Liverpool ndio hawakuwa tayari kumuuza nyota huyo kutoka Uruguay. Chanzo: binzubeiry

No comments:
Post a Comment