Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi yaelezea kuhusu mikakati ya Serikali;
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakitazama moja ya
mabwawa yanayotumika kufugia samaki katika mradi unaoendeshwa na
William Bwemelo katika eneo la Pugu Kinyamwezi kwa msaada wa Wataalamu
wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari akiwaeleza waandishi wa habari
kuhusu mikakati ya Serikali katika kukabiliana na upungufu wa samaki
nchini kwa kutoa msukumo kwa wananchi kuanzisha miradi ya ufugaji wa
samaki katika maeneo yao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu Zahor El Kharousy.(P.T)
Baadhi ya Waandishi wa habari
wakisikiliza maelezo toka kwa Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari akiwaeleza kuhusu mikakati ya Serikali
katika kukabiliana na upungufu wa samaki nchini wakati walipotembelea
moja ya miradi ya ufugaji samaki katika eneo la Pugu Kinyamwezi jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo
ya Uvuvi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Fatma Sobo
akiwaeleza waandishi wa habari juu hatua zinazochukuliwa na Serikali
katika kupambana na Uvuvi haramu hapa nchini.
Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya
Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dr. Baraka Kuguru akifafanua kwa waandishi wa
habari namna bora ya kukuza vifaranga vya samaki wakati walipotembelea
mradi huo.
No comments:
Post a Comment