TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, September 24, 2013

MAMA KIKWETE AKIOMBA CHUO KIKUU KUFUNDISHA LUGHA YA KISWAHILI 

salma d6309
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi. (HM)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba chuo kikuu cha Monmouth cha mjini New Jersey nchini Marekani kufundisha wanafunzi wake lugha ya Kiswahili kama lugha ya kigeni ili wakazi wa eneo hilo waweze kuitumia katika mawasiliano pale itakapohitajika.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ametoa ombi hilo leo wakati akiongea na uongozi wa chuo hicho alipowatembelea yeye na ujumbe wake.
Alisema hivi sasa lugha ya kiswahili inakuwa kwa kasi na kutumika katika maeneo mengi hasa nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi nao wawafundishe wanafunzi wao ili wakienda katika nchi hizo iwe ni rahisi kwao kuwasiliana.

"Kiswahili ni lugha ya taifa letu la Tanzania ambayo tunaitumia katika mawasiliano, mkiwafundisha wanafunzi wenu lugha hii nao watawafundisha wenzao hivyo itakuwa ni rahisi kwao kuwasiliana hasa wakisafiri na kukutana na watu wanaotumia lugha hii", alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake makamu rais wa chuo hicho Dk. Edward Christensen alimshukuru mama Kikwete kwa kutembelea chuo hicho na kusema kuwa ombi lake la chuo hicho kufundisha lugha ya Kiswahili wamelisikia na wataangalia jinsi gani watalifanyia kazi.
Aidha Dk. Christensen aliwaomba wakufunzi na watu wenye utaalamu wa mambo mbalimbali kutoka nchini Tanzania kwenda katika chuo hicho kufanya midahalo na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kinawanafunzi wapatao 6300 kutoka ndani na n je ya nchi 29 na kinatoa kozi mbalimbali zikiwemo za Sayansi na sanaa katika ngazi ya cheti, shahada na shahada ya uzamili. Chanzo: Anna Nkinda

No comments:

Post a Comment