MISS UTALII KUTANGAZA KUPATIKANA NYATI WA AJABU NGORONGORO
Nyati mweupe nayepatikana Ngorongoro (HM)
Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said
Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee
duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha
pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya
Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza
kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss
Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial
Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu
Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu
ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya
pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake ,
kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia
Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater pamoja na maajabu ya bonde
lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo
wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila
mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai,
lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama
katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama
wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu,
Kaka kuona n.k.
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya
Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo
tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze kuingiza
pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na
kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza
utalii na kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza
mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa
majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika
hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya
tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la mamlaka wakienda kazini
walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando ya
barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa
basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao
kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera
walizokuwa nazo.
Hadija ameushukuru uongozi wa
Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya hifadhi hiyo,ambazo
atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo vya Televisheni vya
nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya Miss Tourism
World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na dunia
nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism
Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Chanzo:
fullshangweblog
No comments:
Post a Comment