TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, September 18, 2013

RAIS WA BRAZIL AFUTILIA MBALI ZIARA MBALI ZIARA YA MAREKANI

Dilma_Rousseff_Barack_Obama_2012_0_c7472.jpg
Rais wa Brazil Dilma Rousseff amefutilia mbali mpango wake wa kusafiri nchini Marekani mwezi ujao kutokana na madai kuwa Marekni ilikuwa inaipeleleza nchi hiyo.
Shirika la usalama wa kitaifa la Marekani (NSA) limetuhumiwa kwa kunasa kisiri barua pepe na ujumbe mwingine kutoka kwa Rais Rousseff, wasadizi wake na shirika la kitaifa la mafuta ,Petrobras. (HM)
Madai hayo yalitokana na stakabadhi zilizofichuliwa na aliyekuwa afisaa wa ujasusi nchini Marekani Edward Snowden.
Rais wa Marekani Barack Obama aliahidi kuchunguza kisa hicho.
Ikulu ya White House iliwasiliana kwa njia ya simu na Rais Rousseff mnamo siku ya Jumatatu kujadili swala hilo.
Madai dhidi ya Marekani kuwafanyia udukuzi raia wa Brazil yalichapishwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai na mwandishi wa habari wa jarida la Uingereza la Gurdian, nchini humo.
Greenwald alidai kuwa shirika la NSA liliweza kunasa taarifa zote za kuonyesha kuwa Bi Rousseff alikuwa kwenye mtandao. Chanzo: bbcswahili

No comments:

Post a Comment