TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, September 24, 2013

TANZANIA YATWAA UBINGWA AIRTEL RISING STARS

TIMU ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu nchini Nigeria, baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 katika Fainali.
zzTanzanian_Captain_CEO_and_Tanzanian_Coach_1_8d5da.jpg
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania kwa kufunga bao hilo pekee la ushindi jana.
Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone, Malawi, na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1, wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.
zzzzPict_2_68552.jpg
Malkia wadogo; Tanzania wakiwa na Kombe lao baada ya ushindi (P.T)
Katika Robo Fainali, mabinti wa kibongo wakashinda 4-2 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya DRC Uwanja wa NIS Sports, kabla ya kuifumua Uganda kwa mabai 8-1 kwenye Nusu Fainali.
Mbali na ushindi huo wa wasichana wa Tanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.
Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6 katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.
CEO_AND_TANZANIAN_CAPTAIN_Stumai_Abdallah_1c92d.jpg
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria, Segun Ognsanya Katikati akimkabithi Nahodha wa timu ya wasichana Tanzania, zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Pict_3_8bc24.jpg
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Pict_5_dea50.jpg
Mabingwa; Kikosi cha Tanzania wanawake
Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita. Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.
Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo
Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main Bowl.
Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu na yamekua bora kwa vijana wadogo na kwa kuzingatia jinsia.
Chanzo:http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment