TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, September 23, 2013

ARSENAL YAITANDIKA STOCK CITY 3-1

arsenal 8f453
Ramsey akishangilia na wachezaji wenzake (HM)
arsenal2 b4fa0
MCHEZAJI ghali wa Arsenal, Mesut Ozil ameendelea kulipa Pauni Milioni 43 zilizotolewa kumnunua kutoka Real Madrid baada ya kutoa pasi zote za mabao matatu, The Gunners ikishinda 3-0 Uwanja wa Emirates dhidi ya Stoke City na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England.
Aaron Ramsey alifunga bao lake la saba msimu huu dakika ya tano baada ya akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ozil, lakini Geoff Cameron akaisawazishia Stoke dakika ya 26.
Ozil akadhihirisha yeye ni mkali, baada ya mpira wa kona aliopiga kuunganishwa kimiani kwa kichwa a Mjerumani mwenzake, beki Per Mertesacker dakika ya 36 kuipa Arsenal bao la kuongoza.
Ozil tena akamtengenezea Bacary Sagna nafasi ya kufunga bao la tatu dakika ya 72.
Huu unakuwa ushindi wa saba mfululizo kwa Arsenal tangu wafungwe 3-1 nyumbani na Aston Villa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere/Monreal dk73, Ramsey, Gnabry/Ryo dk73, Ozil/Arteta dk81, Giroud.
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Pieters/Palacios dk67, Wilson, N'Zonzi, Adam/Ireland dk59, Walters, Arnautovic, Jones/Pennant dk75. Chanzo: Sportma

No comments:

Post a Comment