TRA kutoa adhabu kwa wasiotumia EFD ifikapo Novemba
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)
imetangaza kuwa ifikapo Novemba 15 mwaka huu wafanyabiashara wote
watalazimishwa kutumia risiti za kielektroniki ikiwa ni mkakati wake
wakuongeza mapato. (HM)
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye hoteli ya MR, Manispaa ya Iringa, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu
kwa walipa kodi, Richard Kayombo alisema muda wa hiari wa kuanza kutumia
mashine hizo ulianza Mei na unaisha Novemba 15 mwaka huu.
Alisema kuanzia hapo wafanyabiashara watalazimika kununua mashine hizo kwa lazima sambamba na kuchukuliwa hatua ikiwemo kutozwa faini.
Alisema matumizi ya mashine hizo yameonesha mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza makusanyo.
Kayombo alisema fedha ambazo zinatumika kununulia mashine hizo zinarudi kwa mfanyabiashara kwa kupunguzwa kwenye kodi taratibu mpaka inapokwisha.
Aidha Kayombo alisema wameanzisha mfumo wa kulipia ada za magari kwa kutumia simu M pesa, Tigo pesa na Airtel Money ambapo wameweza kukusanya fedha nyingi tofauti na makusanyo yaliyofanywa mwaka jana.
Alisema kwa kipindi cha wiki tatu za Agosti wameweza kukusanya Sh4.7Bn ada za magari tofauti na makusanyo ya kipindi kama hicho mwaka jana ambapo walikusanya Sh3.6Bn.
Alisema kumekuwepo na ongezeko la Sh1.1Bn jambo ambalo linaonesha mafanikio katika matumizi ya mashine hizo.
Aliyataja mambo matatu yaliyokatika mkakati wa miaka mitano wa TRA kuwa ni pamoja na kurahisisha ulipaji wa kodi, kuhakikisha wote wanalipa kodi na wanalipa kwa wakati na kuboresha mfumo wa utendaji. Chanzo: Hakimu Mwafongo

No comments:
Post a Comment