Jumuiya ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate
Jumuiya
ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate, Siku nane tangu kutokea
kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na
kujeruhi wasiopungua 175.
MC
Humphrey OneMic Muturi akiwa Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial
Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya kuomboleza mauwaji ya Westgate.
Wakenya kutoka sehemu mbalimbali duniani wameungana na wenzao katika maombi na ishara za matumaini kwa wenzao wa nchini Kenya.(P.T)
Baadhi ya
waKenya kutoka sehemu mbalimbali hapa DMV Siku ya Jumapili Sept 29
walikutana Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini
Washington, D.C kwa maombolezo ya mauwaji yaliotokea jijini Nairobi siku
ya Jumamosi Sept 29 ndani ya Westgate Mall jijini Nairobi Kenya.
Pastor
Maurice Kinyanjui akifungua hafla hiyo kwa dua maalumu ya maobolezo ya
mauwaji ya Westgate yaliofanyika Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln
Memorial Jijini Washington, D.C
Jumuiya ya
waKenya na rafiki wa wanajumuia hao walikutana Mbele ya mjengo wa
Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya
kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapa matumaini wenzao walioathirika na tukio
hilo.
Walianza
kwa ufunguzi kuwaombea dua walioathirika na tukeo hilo lilitokea Siku ya
Jumamosi Sept 21, ambapo kundi la Al shabab walivamia na kuteka eneo la
sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate Mall Jijini Nairobi Kenya
Waliendelea
kwa kukumbushana mengi yakiwemo kusisitiza kwa upendo wa kua kitu
kimoja bila ya kujali tafauti zao na kuvumilia kwa yote yaliotokea kwani
Kenya ni nchi ya amani.
Siku nane tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na kujeruhi wasiopungua 175.
No comments:
Post a Comment