TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, September 28, 2013

UTPC YAJIPANGA KUISHTAKI SERIKALI KWA MAUAJI

karsan e3347
UMOJA Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umesema jopo la wanasheria wake lipo katika hatua za mwisho za kuandaa mashitaka dhidi ya Serikali kutokana na mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi. (HM)

Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan alipozungumza na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Karsan alisema Serikali itafunguliwa mashitaka ya madai kwa kuwa askari wake ndiyo waliotekeleza tukio la kinyama dhidi ya Mwangosi wakati akitimiza majukumu yake.
"Baada ya tukio lile la Septemba 2,2012, UTPC hatukutaka kuanza kulumbana na Serikali bali tulianza kushughulikia kwanza familia ya marehemu Mwangosi ili kurudi katika hali yake ya kawaida.
"Tumefanikiwa kuiweka familia yake katika hali nzuri ya uchumi kwa kuanza kumwanzishia mke wake mradi wa zaidi ya Sh milioni 10 ambao anaendelea nao mpaka sasa, pia tuanzisha mfuko wa maalum wa Daudi Mwangosi Fund.
"Mfuko huu utakuwa maalum kwa waandishi wote watakaopatwa na matatizo ya aina yoyote yake, pia kila mwaka Septemba 2 tutakuwa tunatoa tuzo Sh milioni 10 kwa mwandishi bora.
"Sasa msimamo wa UTPC ni kutaka Serikali itoe malipo kwa familia ya marehemu Mwangosi, hatufungui kesi ya jinai la hasha kwa sababu hatua za sheria kwa askari waliohusika zinachukuliwa," alisema.
Mauaji ya Mwangosi yalitokea Septemba 2, 2012 eneo la Nyololo wa katika ufunguzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kuibuka ghasia polisi walipoamuru wafuasi wa chama hicho kutawanyika katika ufunguzi wa tawi hilo.
Katika hatua nyingine, UTPC imepiga marufuku waandishi wa habari kuomba au kupokea posho kutoka kwa wadau wa habari ispokuwa tu pale anapotoa kwa hiari yake. Chanzo: mtanzania

No comments:

Post a Comment