-Alikuwa mke wa Lindsay, mtuhumiwa wa ugaidi jijini London
-Alikuwa anatafutwa na polisi wa Kenya kabla ya tukio la juzi
-Al-Shabaab wamtaja kuwa mwanamke shujaa
-Alipanga kumtorosha mwenzake aitwaye Grant leo
Habari: Clarence Mulisa na Mitandao
MWANAMAMA Samantha Lewthwaite amehusishwa katika shambulio la kigaidi lililotokea jijini Nairobi, juzi Jumamosi kwenye jengo la biashara la Westgate.
Lewthwaite anadaiwa kuwa miongoni mwa 
magaidi 10-15 waliohusika katika tukio hilo lililopoteza maisha ya watu 
69 mpaka sasa wakati zaidi ya 175 wakijeruhiwa.
Mume wa Lewthwaite, Germaine Maurice Lindsay aliyeua watu 26 katika mlipuko wa Julai 7, 2005 jijini London.
Samantha Lewthwaite (29), maarufu kama 
'Mjane Mweupe' ni Mwingereza aliyekuwa mke wa Germaine Maurice Lindsay 
maarufu kwa jina la Abdullah  Shaheed Jamal, mmoja wa magaidi kati ya 
wanne waliojitoa mhanga katika shambulio la Julai 7, 2005 jijini London 
lijulikanalo kama (7/7) lililoua watu  56 pamoja na wao na kujeruhi 
zaidi ya 700.
Bomu la  Lindsay liliua watu 26 baada ya kulipua treni ipitayo chini ya ardhi jijini London.
Lewthwaite, ambaye alibadili dini enzi za ujana wake na kuitwa Sherafiyah anadaiwa kuwa na watoto watatu.
Lewthwaite, ambaye alibadili dini enzi za ujana wake na kuitwa Sherafiyah anadaiwa kuwa na watoto watatu.
Serikali ya Kenya imeeleza kuwa baadhi ya 
majeruhi waliookolewa kutoka katika jengo la Westgate walidai kumuona 
mwanamke mweupe (aliyefanana na Lewthwaite)  akiwa miongoni mwa magaidi 
walioteka jengo hilo.
Al- Shabaab kupitia katika akaunti yao ya 
Twitter wamemtukuza Lewthwaite kwa kusema yupo katika viwango vyao na 
ni  mwanamke shujaa.
Inasadikiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa 
mmoja kati ya viongozi wa magaidi hao baada ya askari kudai kuwa 
mwanamke mweupe aliyekuwa amevaa hijabu alikuwa akitoa amri kwa wenzake 
katika lugha ya Kiarabu wakati wa shambulio hilo.
Desemba 2011, askari nchini Kenya walibaini
 kemikali za kutengeneza milipuko sawa na zile zilizotumika katika 
milipuko ya Julai 7, 2005 jijini London katika vyumba viwili vya 
kupangisha. Lewthwaite alidaiwa kuwa ndiye aliyekuwa amepangisha vyumba 
hivyo japo hakukamatwa.
Katika tukio hilo, Mwingereza, Jermaine 
Grant, alikamatwa akiwa jijini Mombasa kwa kuhusika na kemikali hizo. 
Baada ya kukamatwa, Grant aliwaeleza askari wa Kenya kuwa anafanya kazi 
chini ya Lewthwaite. Alikamatwa pamoja na mtu mwingine aliyekuwa 
anajaribu kutoroka nchini Kenya.
Habari
 iliyotolewa na gazeti la The Sun la Septemba 23, 2005 ikiwa na picha ya
 Lewthwaite akiwa amembeba mwanaye wa kike Ruqayyah, aliyezaa na 
Lindsay.
Aprili 2012, ilithibitishwa kuwa mtuhumiwa 
katika tukio hilo alikuwa Lewthwaite mwenyewe ambaye anadaiwa kuvuka 
mpaka wa Kenya na kuja Tanzania akiwa na watoto wake watatu Desemba 26, 
2011.
Machi mwaka huu, Daily Telegraph liliripoti kuwa Lewthwaite na Fouad 
Manswab walikuwa wanapanga kumtorosha Grant na mpango wao ulipangwa 
kufanyika leo Septemba 23, 2013 jijini Mombasa."Tunajua Fouad anawasiliana na Samantha Lewthwaite na walipanga kumuokoa mwenzao," alisema Jacob Ondari, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa Kenya kipindi hicho.
Katika ripoti mbalimbali, Lewthwaite anatajwa kuwa mfadhili, muongozaji na mwalimu wa Al Qaeda na muandaaji wa Kundi la Jihad kwa wanawake barani Afrika.




No comments:
Post a Comment