SWANSEA YAICHAPA VALENCIA 3-0 EUROPA LEAGUE

Swansea wakishangilia bao
WAKALI wa soka ya kitabuni England, 
Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 
nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10. (HM)
Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa 
takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi 
nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia 
Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la 
tano katika mechi nanemsimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita, 
Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi 
Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga.
Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56, 
Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65, 
Michu/Shelvey dk77 na Bony.
Katika mchezo mwingine, mabao mawili 
ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso,
 bao lingine akifunga Christian Eriksen.

Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji
 10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre 
Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut, 
Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred, 
Ondrasek. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment