BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU ITALIA KWA KUMVAGAA REFA
Mario Balotelli akitulizwa na wachezaji wenzake (HM)
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli
amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo ambao timu yake,
AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.
Balotelli, ambaye alikosa na kufunga
bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake, alionyeshwa kadi ya pili ya
njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.
Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
Balotelli, ambaye alifunga penalti
zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, mkwaju wa Jumapili uliokolewa
na kipa wa Napoli, Pepe Reina.
Kadi hiyo nyekundu ya utata,
inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna, Sampdoria na Juventus,
ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment