MOURINHO AAGA KWA KISHINDO, MADRID YAITWANGA OSASUNA 4-2
Mourihno
Mourihno
Ronaldo akipunga mkono jambo ambalo limewashangaza na kuwastua mashabiki wa Madrid
Mourihno akimpa maelekezo Essien
KOCHA Jose Mourinho jana aliwaaga
mashabiki wa Real Madrid katika mchezo wa mwisho wa La Liga alipokea
kelele za kushangiliwa na kuzomewa wakati timu yake ikiifunga Osasuna
4-2 Uwanja wa Bernabeu.
Lakini kulitokea sintofahamu kuhusu
mustakabali wa mchezaji anayewaniwa na Manchester United na Chelsea,
Cristiano Ronaldo, ambaye aliikosa mechi hiyo kutokana na kuwa
majeruhi.
Kocha huyo Mreno alitoa taarifa fupi ya kuaga katika tovuti ya Madrid saa chache kabla ya mechi na Osasuna.
Baada ya mechi, Mourinho, ambaye
anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kurejea Chelsea msimu ujao,
aliwapungia mkono mashabiki kuwaaga kabla ya kuondoka uwanjani.
Mourinho, ambaye katika maisha yake ya
ukocha anajivunia kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na ubingwa
wa Ligi za Ureno, England, Italia na Hispania Spain anatarajiwa kurejea
Chelsea msimu ujao.
Baada ya kushinda Kombe la Mfalme
katika msimu wake wa kwanza na Ligi Kuu ya Hispania katika msimu wa
pili, Mourinho na klabu zilikubaliana kuachana baada ya msimu huu wa
tatu.
Mourinho amekuwa akishambuliwa mno kwa
kumuweka benchi Nahodha na kipa Iker Casillas msimu huu na akionekana
kuwapendelea baadhi ya wachezaji kama Pepe.
Wachezaji wengine wa Madrid wamemtakia kila la heri Mourinho.
Katika mchezo wa jana, Gonzalo Higuain
aliifungia Madrid bao la kuongoza dakika ya 35, kabla ya Michael Essien
kufunga la pili dakika nne baadaye.
Osasuna ilisawazisha kupitia kwa Roberto Torres na Alvaro Cejudo.
Karim Benzema akaisawazishia Real
zikiwa zimesalia dakika 20 kabla ya bao la dakika za lala salama la Jose
kuihakikishia ushindi Madrid.
No comments:
Post a Comment