WANAFUNZI TISA WAUAWA NA BOKO HARAM
Washukiwa
wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, wamewaua wanafunzi
tisa , katika shambulizi la pili ambalo limewalenga wanafunzi katika
siku za hivi karibuni.
Washambuliaji wanaoaminika kuwa
wanachama wa kundi la wapiganaji wa Boko Haram, waliwashambulia kwa
risasi wanafunzi hao waliokuwa wamevalia sare za shule katika shule moja
viungani mwa mji wa Maiduguri.
Boko Haram ilikiri kufanya mashambulizi hayo na kusema ilikuwa adhabu kwa vijana kwa kuunga mkono jeshi.
Baadhi ya manusura walisema kuwa ilikuwa hatua dhidi ya kuibuka kwa makundi ya vijana wanaotoa ulinzi kwa raia mjini humo.
Eneo la Kaskazini mwa Nigeria, liko chini ya sheria ya hali ya hatari huku serikali ikijaribu kupambana na kundi la Boko Haram pamoja na harakati za makundi ya kiisilamu.
Mmoja wa walioshuhudia Ibrahim Mohammed alisema alikuwa darasani akifanya mtihani wakati watu hao walipovamia jengo hilo.
"niliona wanafunzi watano, waliokuwa wanafanya mtihani wakiuawa papo hapo.''
''Wanafunzi wengine, waliuawa walipokuwa wanaingia shuleni''
Wafanyakazi wa hospitalini walithibitisha kuona miili ya watoto tisa wakiwa bado wamevalia sare zao wakipelekwa katikia chumba cha kuhifadhia maiti Maiduguri.
Msemaji wa Boko Haram, aliwaambia waandishi wa habari kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi na onyo kwa vijana kwa kusaidiana na jeshi.
Makundi ya vijana wanaotoa ulinzi wamekuwa wakiwakamata washukiwa wa Boko Haram na kuwakabidhi kwa jeshi.
Msemaji wa jeshi alisema kuwa wale waliokabidhiwa kwa polisi watafikishwa mahakamani na kutendewa haki. Chanzo:bbcswahili

No comments:
Post a Comment