WOLPER NA HALIMA MDEE WANATARAJIWA KUTOANA MANUNDU USIKU WA MATUMAINI
MSANII
wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameenda kujichimbia Afrika Kusini
akifanya mazoezi ili ajiweke katika nafasi ya kuzichapa na mbunge wa
CHADEMA Halima Mdee, katika tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7
mwaka huu.
Wolper ambaye atapigana na Halima Mdee, alisema kuwa
amejikita nchini humo kwa ajili ya kujiweka sawa ili aweze kumkabiri
mbunge huyo.
Alisema mbali ya kujiweka fiti kwa ajili ya
kumkabili mbunge huyo pia anajiweka fiti kwa ajili ya kujenga mwili wake
ili kupunguza magonjwa pamoja na kujinginga na magonjwa ya kisukali
yanayotokana na mafuta.
"Naamini nitamgaragaza mbunge huyo na
sitochukua hata dakika tano kwenye mchezo huo kwani naamini mazoezi
yangu ninayoyafanya ni njia moja wapo ya kujiweka vizuri kimwili"
alisema Wolper.
Siku ya Usiku wa Matumaini utapambwa na
mashindano kibao yakiwemo mbunge wa viti maalumu Ester Bulaya ambaye
naye anatarajia kuzichapa na Aunt Ezekiel, huku Zitto Kabwe atazichapa
na Vincent Kigosi
No comments:
Post a Comment