MWANDISHI WA HABARI BURUNDI AKAMATWA
Viongozi nchini Burundi wamethibitisha kukamatwa kwa mmoja wa watangazaji wa Televisheni moja nchini humo pamoja na watu wengine watatu siku ya Alhamis.
Msemaji wa Idara ya usalama wa taifa 
ya Burundi, Telesphore Bigirimana amesema mwandishi huyo Lucien Rukevya 
hajawahi kushitakiwa kwa makosa yoyote ya jinai lakini anashikiliwa kwa 
kuvunja sheria za usalama wa nchi.
        
Msemaji huyo aliendelea kwa kusema 
watu wengine watatu wanaoshikiliwa ni ni waziri wa zamani Ignace 
Bankamwabo na watu wengine wawili raia wa Congo ambao wanadhaniwa kuwahi
 kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 la Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo.
Chama cha waandishi wa habari nchini Burundi kimesema bwana Rukevya ni mwandishi wa tatu nchini humo kukamatwa tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata mwanzoni mwa mwezi huu. Chanzo: bbcswahili
                    
Chama cha waandishi wa habari nchini Burundi kimesema bwana Rukevya ni mwandishi wa tatu nchini humo kukamatwa tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata mwanzoni mwa mwezi huu. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment